Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh amenukuliwa akisema hayo na shirika la habari la Fars na kuonya kuwa, Iran haitasita kutoa jibu kali lenye kuumiza kwa hatua yoyote ya kichokozi ya adui.
Brigedia Jenerali Hajizadeh amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni taifa kubwa na lenye uwezo mkubwa, jambo ambalo linawatia kiwewe maadui.
Amebainisha kuwa, "iwapo kutatokea uvamizi wowote dhidi ya Iran, hakuna shaka kuwa jibu la Jamhuri ya Kiislamu kwa uchokozi wa maadui litakuwa kali, na kwa msingi huo hawapaswi kufanya kosa hilo la kimahesabu."
Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza bayana kuwa, Iran imepiga hatua kubwa ya kujitosheleza katika uga wa ulinzi, na hii ni stratejia ya ushindi iliyochukuliwa na Iran dhidi ya madola ya kibeberu.
Jenerali Hajizadeh ameongeza kuwa, motisha na ari ya juu ya vikosi vya ulinzi vya Ira imelifanya taifa hili lipate mafanikio mengi, chini ya miongozo na maelekezo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapindizi ya Kiislamu, Ayatulah Sayyid Ali Khamenei.
342/